Fashion

BODI YA MIKOPO YAONGEZA SIKU

erisak | 4:58 AM | 0 comments


 Image result for BODI YA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha maombi yao hadi mwishoni mwa mwezi huu (31 Julai, 2015).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano, Julai 15, 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Bw. George Nyatega, hatua hiyo imechukuliwa ili kuwapa fursa wombaji ambao hawajakamilisha kufanya hivyo.

“Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika  muda uliopangwa,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari.

 Itakumbukwa kuwa awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015.

Kupitia taarifa yake, HESLB imewataka waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015.

SOURCE: HESLB

Category: ,

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments